VUNJO: Mbatia ambwaga vibaya Augustine Mrema


Tume ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza James Mbatia wa NCCR Mageuzi kuwa mbunge mteule wa jimbo la Vunjo huku kada wa Chadema, Anthony Komu naye akiibuka mshindi katika jimbo la Moshi Vijijini lililokuwa linaongozwa na Waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda, Dk. Cyril Chami kupitia CCM.

Akitangaza matokeo ya majimbo hayo mawili mkoani Kilimanjaro kuamkia leo, msimamizi Fulgence Mponji, amesema Mbatia amepata kura 60,187 akiwashinda wapinzani wake; Innocent Shirima wa CCM aliyepata kura 16,617 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata kura 6,416.

Kutokana na matokeo hayo,  Mrema ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Vunjo huku wananchi wa eneo hilo wakiendeleza historia ya kutomchagua mbunge wa chama kimoja kwa vipindi viwili tangu kurudi kwa mfumo wa siasa za vyama vingi.

Kwa mujibu wa Mponji, mbunge mteule wa Moshi Vijijini, Komu amepata kura 55,813 huku Dk Cyril Chami akijikusanyia kura kura 24,415.
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com