Bosi wa Chelsea Jose Mourinho amekiri kuwa kutetea
ubingwa msimu huu ni kitendawili kwa miamba hao wa London wenye maskani
yao Darajani Stamford Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho alicharukia maswali ya waandishi wa
habari kuhusu mustakabali wake akisisitiza kuwa kama klabu itamtupia
virago, watakuwa wanamfukuza meneja bora ambaye klabu haijawahi kuwa
naye.
Mabingwa hao watetezi walipokea kipigo cha nne ligi kuu ya Uingereza
msimu huu katika mechi iliyopigwa Jumamosi, wakilala kwa magoli 3-1
dhidi ya Southampton, tena katika uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge
licha ya kutangulia kupata goli dakika ya 10 kupitia Willian.
Kipigo hicho kimeongozana na kichapo cha 2-1 walichopokea Jumanne
kutoka kwa Port Ligi ya Mabingwa Ulaya. Chelsea sasa inashika nafasi ya
16 katika msimamo wa ligi ya Uingereza wakiwa wameachwa pointi 10 na
vinara wa ligi hiyo Manchester City. “Kama klabu inataka kunifukuza wanifukuze tu kwa sababu sitakimbia,” alikiambia Sky Sports baada ya mchezo
"Kuwa mabingwa kwa sasa ni vigumu sana kwa sababu umbali umekuwa mrefu
sana lakini bado nina imani tunaweza kumaliza tukiwa nafasi nne za
mwanzo.
“Mwezi Desemba, Januari na Februari tutakuwa ndani ya nne bora"
“Ni wakati muhimu sana katika historia ya klabu hii kwa sababu kama
wakinifukuza kazi watakuwa wanamfukuza meneja bora mno aliyewahi kuinoa
klabu hii” aliongeza Mourinho.
“Ujumbe ni kwamba matokeo mabaya ni kwa sababu ya uzembe wa meneja.
Huu ni wakati wa kila mmoja kutambua majukumu yake na kutoa ushirikiano
na kuwa na umoja.”
Mourinho pia alilalamika kuwa Chelsea hawakutendewa haki na waamuzi
na amedai kuwa walinyimwa penalti dhidi ya Southampton, ambayo anaamini
ingebadili matokeo ya mchezo.
“Waamuzi wanaogopa kutoa maamuzi ya kuipa haki Chelsea,” aliongeza.
“Wakati tukiwa 1-1, tulipata penalti ya wazi lakini hatukupewa".
“Kama FA wanataka kuniadhibu wafanye hivyo. Hawaadhibu mameneja wengine. Wachezaji wangu wanastahili haki, na mashabiki pia".
“Waamuzi wanaogopa kuitendea Chelsea haki. Kwanini? Mara zote kuna
alama ya kiulizo isiyo na jibu, na huwa tunaishia kuadhibiwa tu".
“Penalti za wazi kabisa hazitolewi. Hata mechi ya Ligi ya Mabingwa
tuliyofungwa 2-1, hatukupewa penalti tuliyostahili kuipata dakika ya
mwisho".
“Penalti katika mchezo huu ilikuwa muhimu kwa sababu kipindi hiki
timu yangu imefungwa kwa kunyimwa haki. Penalti nzuri kabisa ya wazi
tumenyimwa na baada ya hapo timu ikaanza kupoteana, kukosa kujiamini
hatimaye kila kitu kikaenda mrama”
Chanzo: Goal.com
Sign up here with your email