Mwanasiasa Mkongwe Mheshimiwa Kingunge Ngombare Mwiru leo ametangaza kujiondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na sasa atakuwa mwananchi huru.
Kingunge amezungumza leo mbele ya
waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake Kijitonyama, Dar es salaam. Amesema
kutokana na matukio yaliyotokea katika kumpata mgombea Urais kupitia chama
chake ni tofauti na ilivyokuwa mwaka 1995 na 2005 hivyo ameamua kuondoka ndani
ya chama hicho na sasa yupo huru.
Kingunge amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na
kile alichoamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa Misingi bora
na waasisi wake. Aidha amesema hakusudii kujiunga na Chama Chochote cha
Siasa nchini bali atakuwa mtanzania huru.
Kingune amesema hawezi kuhimili
chama kisichojiendesha bila katiba na anajua uamuzi wake utawasumbua baadhi ya
ndugu zake, wazee na makada wengine. Mwanasiasa huyo amesema kwa sasa hakusudii
kujiunga na chama kingine chochote kwa kuwa amekuwa mwanaharakati kwa miaka 61.
Pia amesema yeye ni raia na ana haki
zake za kisiasa na kijamii na ataendelea kuwa na mahusiano mazuri na nchi yake.”Hali ya sasa jinsi ninavyoona vijana,
wafanyakazi, wakulima wanataka mabadiliko na mimi nipo upande wa mabadiliko kwa
sababu wakati tukiwa TANU tulifanya mabadiliko na kuunda CCM”…KINGUNGE
Akizungumzia hali ya sasa kisiasa amesema kila kipindi
katika jamii ya kitanzania hivi sasa inataka mabadiliko. Kingunge ametangaza uamuzi
wake huo hivi pinde katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao unarushwa
moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ITV.
Sign up here with your email