MIHURI YA 2010 YATUMIKA KUMAKI KARATASI ZA KURA

MIHURI YA 2010 YATUMIKA KUMAKI KARATASI ZA KURA

Upigaji kura katika baadhi ya vituo Manispaa ya Morogoro umeingia dosari kutokana na baadhi waandikishaji kulazimika kutumia mihuri ya mwaka 2010 baada ya ile ya sasa kugoma hali iliyozua malalamiko miongoni mwa wagombea ubunge.
Akizungumzia tatizo hilo la mihuri, mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Morogoro Mjini ambacho kinaungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Marcossy Albaniel, alisema upigaji kura ulimekwenda vibaya kutokana na kutumika kwa mihuli ya chaguzi zilizopita bila wao (wagombea) kushirikishwa.
Alizitaja baadhi ya kata zilizokumbwa na tatizo hilo la mihuri kuwa ni vya kata za Mazimbu na Kihonda hali iliyopelekea kuchelewa kuanza kwa upigaji wa kura.
Albaniel alisema baada ya kutokea kwa hali hiyo waliwasiliana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi lakini alishindwa kutoa majibu na badala yake kuamua kutumia mihuri hiyo bila kuwashirikisha wagombea wala viongozi wa vyama.
“Tumejaribu kumpigia simu msimamizi wa uchaguzi wa manispaa lakini simu zetu hapokei, kwakuwa amebadilisha utaratibu bila kutushirikisha na sisi tunasema hatutaki mihuri hiyo iendelee kutumika,” alisema Albaniel.
Mbali na hilo mgombea huyo alidai Jeshi la Polisi lilikuwa likiwakataza wagombea kuingia katika vituo vya kupigia kura kuangalia jinsi shughuli hiyo ilivyokuwa ikiendelea kinyume na utaratibu uliowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Morogoro, James Mkude, alisema ameshangazwa na msimamizi huyo wa uchaguzi kujichukulia uamuzi wa kubadilisha mihuri bila kuwashirikisha wao kama viongozi wa chama kilichosimamisha wagombea.
Naye mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Wakulima (AFP), Mark Isdory, alisema hawakubaliani na kitendo kilichofanywa na msimamizi wa uchaguzi wa Manispaa ya Morogoro kubadilisha mihuri ya kupigia kura bila kuwashirikisha na kwamba wanahisi kuna vitendo vya hujuma.
Chanzo: IPP media.

Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com