Umoja usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania unajulikana kwa jina la Katiba ya Wananchi (UKAWA). Mshika bendera wa muungano wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu
ujao ambaye pia alikuwa ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa .
Hii inatokana na sheria za Tanzania ambayo haitambui umoja wa vyama. Kabla
ya kujiengua chama Tawala chama cha Mapinduzi CCM, Edward Lowassa
amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda wa miaka 38, ambapo alijiunga na
chama hicho mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka
1977.
Hatua ya mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Tanzania kuamua
kujiunga na chama cha upinzani Chadema, ikiwa imebaki miezi mitatu tu
kuelekea uchaguzi mkuu, imebadilisha kabisa upepo wa kisiasa nchini
Tanzania, na hasa uchaguzi mkuu ujao.
Lowassa alikuwa Maziri Mkuu kati ya mwaka 2005 na 2008 kabla ya
kujiuzulu wadhifa huo kufuatia kashfa ya rushwa iliyohusisha kampuni
ya kuzalisha umeme ya ki-Marekani Richmond Development Company LLC ya
Houston Texas.
Hata hivyo wakati anatangaza kuhamia kwake Chadema,
Lowassa alikanusha katu kuhusika kwa namna yoyote na kashfa hiyo na
kudai kuwa yeye alifuata tu amri kutoka kwa ‘wakubwa’ walio juu yake. “Kama kuna mtu yeyote mwenye ushahidi basi na aende mahakamani ama sivyo anyamaze” alisema Lowassa
Kuhama kwake kunamfanya Lowassa kuwa ndie kiongozi wa kwanza wa ngazi
ya juu kabisa wa CCM kukihama chama hicho tangu kuanza kwa mfumo wa
vyama vingi nchini Tanzania mnamo mwaka 1992.
Mwanajeshi wa zamani
na aliyewahi kupigana wakati wa vita kati ya Uganda na Tanzania mwaka
1978/79, Lowassa aliiambia hadhara kwamba akiwa kama mtu mwenye uchungu
na nchi yake isingekuwa rahisi kubaki ndani ya CCM huku akiona chama
hicho kimepoteza mwelekeo na sifa ya kuongoza nchi.
Lowassa
alikimbilia upinzani baada jina lake kukatwa wakati alipoomba kuwa
mgombea urais kupitia chama tawala CCM katika uchaguzi mkuu ujao
utakaofanyika baadaye mwezi huu .
Wakati mchakato wa CCM wa kumtafuta mgombea wao wa urais ulipoanza, Lowassa ndiye aliyekuwa kinara wa wagombea wote 42.
Kila kona aliyozunguka, mikutano yake ya hadhara ilivutia maelfu ya watu waliomuunga mkono.
Wakati
chama cha CCM kilimtaka kila mgombea apate sahihi za wadhamini 450
lakini Lowassa alipata sahihi za wadhamini zaidi ya 700,000.
Hata hivyo mchujo wa chama ulipofanyika jina lake lilikatwa mapema
kabla hata ya kupelekwa kwenye vikao vya vya juu vya chama hicho. Ambapo
baadae Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli ndiye aliyeibuka kidedea na
kuwa mgombea kupitia chama tawala CCM.
Lowassa ameushutumu
mchakato CCM wa kutafuta mgombea urais akiuita kuwa ulijaa chuki na
mizengwe dhidi yake, hali ambayo aliifananisha na ‘ubakaji wa
demokrasia’ “Nitakuwa mnafiki nikisema bado nina imani na CCM.''
''CCM
niliyoiona Dodoma si CCM niliyokulia”, alisema, na kuongeza “kama
Watanzania hawapati maendeleo kupitia CCM basi wakayatafute nje ya CCM”
Wakati
sakata la Richmond lilipoibuka miaka michache tu iliyopita, Chadema
ilimfanya limsakame Lowassa kuwa ni mmoja wa mafisadi wakubwa nchini.
Lakini
wakati chama hicho kinamkaribisha kuwa mwanachama wao, kiligeuka na
kusema hakuna mtu msafi nchini na kwamba hawawezi kuacha kumpokea
mwanasiasa mwenye mtaji mkubwa wa wafuasi kama Lowassa.
Wakati akiwa Waziri Mkuu, Lowassa alisifika kama mchapakazi hodari na msimamiaji wa moja kwa moja wa shughuli za serikali. Bado anaendelea kufahamika kwa jina la utani la ‘Mzee wa maamuzi magumu’. Moja
ya mafanikio makubwa ya uwaziri mkuu wake ni jitihada kubwa na
mafanikio ya upatikanaji wa fedha za kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Chuo hiki kikuu cha umma kilichopo katikati ya Tanzania kilianzishwa mwaka 2007.
Lowassa
ni mashuhuri pia kwa kusimamia mpango wa serikali uliofanikiwa wa
ujenzi wa shule za kata ambazo uliiletea Tanzania sifa kubwa kwa kutoa
fursa ya watoto wengi kupata nafasi shuleni.
Mtoto wa Mzee Ngoyai
Lowassa, ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa serikali ya kikoloni, Lowassa
ameanza harakati zake za kuwania urais tangu mwaka 1995 lakini
inaarifiwa kwamba rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere
alimkatalia kushika nafasi hiyo.
Wafuasi wa Lowassa wamekuwa wakiyatupilia mbali madai hayo, Ulipofika
uchaguzi wa mwaka 2005, Lowassa hakutaka kuwania urais, lakini badala
yake alimnadi rafiki yake wa siku nyingi Rais wa sasa Jakaya Kikwete
ambaye alipata ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 80.
Sign up here with your email