Njia ya ubingwa nyeupe- Pluijm

  
KOCHA Mkuu wa Yanga Hans van Pluijm ametamba kuwa haoni sababu ya kushindwa kutetea ubingwa wake. Yanga ndio inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 15 na katikati ya wiki hii iliifunga Mtibwa Sugar mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Pluijm alisema mechi zilizokuwa zikimuumiza kichwa ni Simba na Mtibwa na amezishinda hivyo haoni sababu ya kutotetea ubingwa. "Simba kutokana na historia ya kukutana na Yanga na kuifunga nilikuwa naihofia, na Mtibwa nilihofia maana uwanja wa Jamhuri huwa mgumu kwa Yanga, sasa tumeshinda na tuna imani tutashinda mechi zote zilizosalia," alisema kocha huyo raia wa Uholanzi. 

Aidha alisema, anafahamu ugumu wa mechi zilizosalia kwani sasa kila timu inayokutana nayo itakamia lakini anaamini atashinda. "Mikakati yangu na timu yangu ni kushinda mechi zote katika raundi hii ya kwanza, karibu timu zote sumbufu tumezishinda naamini huko kulikobaki tunateremka tu," alisema. "Lakini si kwamba nazizarau timu nyingine hapana, najua mambo yatazidi kuwa magumu maana sasa kila timu itataka kuifunga Yanga na hapo ndipo ugumu unapokuja, lakini nina timu nzuri, tutashinda mechi zote na kutetea ubingwa wetu," alisema.

Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com