BREAKING NEWS: Mch. Christopher Mtikila afariki kwa ajali ya gari mkoani Pwani

   Mch Christopher Mtikira

Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani asubuhi ya leo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 asubuhi ya leo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze. 
 


         Gari iliyokuwa imembeba Marehem Mtikila

Amesema gari alilokuwa amepanda Mtikila lilikuwa linatoka mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya na kupelekwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha Pwani Kwa habari zaidi endelea kufuatilia habari zetu tutakujuza hivi. 

                                Picha ya Marehem Mtikila baada ya ajali

Kwa habri zaidi endelea kufuatilia habri zetu Tzyako.blogspot.com


Chanzo:Global Publisher
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com