![]() |
| Diego Costa |
Kocha wa Uhispania Vicente de Bosque
amemuacha nje mshambuliaji wa timu hiyo Diego Costa kwa mechi mbili za
kufuzu kwa michuano ya mabingwa Ulaya mwaka ujao. Costa anahudumia
marufuku ya mechi moja kwa kupata kadi nyingi za njano na alikuwa
hawezi kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Luxembourg mnamo tarehe 9 mwezi
Octoba.
Del Bosque:Tumeona tusimshirikishe kwa mechi ya pili dhidi ya Ukraine. ''Hachezi
vibaya'',Del Bosque alisema kuhusu Costa,na kuongezea kwamba Uhispania
itamshirikisha katika mechi za usoni iwapo kila kitu kitakwenda sawa. Costa
pia anahudumia marafuku ya mechi tatu nchini Uingereza kwa kusababisha
ghasia katika ushindi wa Chelsea dhidi ya Arsenal baada ya kuweka mikono
yake katika uso wa mlinzi Laurent Koscielny.
''Sikupendelea kile nilichokiona'',Del Bosque alisema kuhusu kisa hicho.''Sipendelei kile Costa alichokifanya''.
Sign up here with your email
