Kiongozi wa mbio za Mwenge wa
Uhuru 2015, Juma Khatib Chum,akizindua mradi wa kilimo cha umwangiliaji
cha vitunguu kijiji cha Nkungi wilaya ya Mkalama.Chum aliagiza vijana
waache kukaa vijiweni na badala yake waelekeze nguvu zao katika shughuli
mbalimbali zitakazowapatia kipato ikiwemo kilimo cha umwangiliaji.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2015, Juma Khatib Chum, akikabidhi baadhi ya misaada ikiwemo simu za viganjani kwa walemavu wa ngozi (Albino) wa wilaya ya Mkalama.
KIONGOZI
wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2015,Juma Khatib Chum,amezihimiza
halmashauri za wilaya, manispaa na majiji nchini, kutenga bajeti kwa
ajili ya kugharamia huduma za watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) kwa
madai kwamba wengi wao hali zao kiuchumi ni duni.
Chum
ametoa wito huo muda mfupi baada ya kukabidhi misaada mbalimbali
ikiwemo kadi za kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwa walemavu wa
ngozi 28 wa wilaya ya Mkalama.Alisema
watu wenye ualbino,wanayo mahitaji maalum mengi ikiwemo mafuta ya ngozi
ambayo gharama yake ni kubwa,hivyo inakuwa ngumu kwao kumudu gharama
hizo.
“Ili
kulisaidia kundi hili dogo la watu wenye ualbino ambao wengi wao
familia zao zina kipato duni,ni halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya
kuwahudumia hawa ndugu zetu”alifafanua Chum.Aidha,
kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru, amemtaka kila Mtanzania kuwa
mlinzi kwa watu wenye ualbino,ili kuwalinda/kuwakinga na watu wenye
lengo la kuwadhuru kutokana na imani zao potofu, kwa viungo vya walemavu
hao,ni dili la kupatia utajiri.
Chum
alitumia fursa hiyo kuishukuru na kuipongeza serikali ya wilaya Mkalama
chini ya DC wake Fadhili Nkurlu kwa ubunifu wao wa kuwasaidia watu
wenye ualbino. “Toka
tumeanza kukimbiza mwenge wa uhuru mwaka huu na sasa tumebakiza mkoa
moja tu tumalize mbio hizi,hatujaona mradi mzuri kama huu wa kuwahudumia
ndugu zetu wenye ualbino”,alisema.
Alisema
kitendo hiki ni kwamba mnajenga mazingira mazuri ambayo yatachangia
ndugu zetu hawa, wajione kuwa na wao ni sehemu ya jamii ya Watanzania. Awali
mkuu wa wilaya ya Mkalama Nkurlu, (kwa sasa amehamishiwa wilaya ya
Arusha) alitaja baadhi ya misaada waliyoitoa kwa walemavu hao wa
ngozi,kuwa ni simu za viganjani na filimbi ambazo zitawasaidia kutoa
taarifa juu ya usalama wao.
Alitaja
mingine kuwa ni kadi ya mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambayo watapatiwa
matibabu kwa mwaka mzima bila ya kuongeza fedha yoyote,na pia wamepatiwa
kofia za kujikinga na mionzi ya jua. “Katika
juhudi za kuimarisha huduma kwa watu wenye ualbino, tunatarajia
kufungua dirisha maalum kwenye vituo vya afya kwa ajili yao kupata
matibabu bila usumbufu.Tutatenga bajeti katika mwaka wa fedha ujao na
tunatarajia kuanzisha miradi mbalimbali kwa ajili ya Chama Cha Walemavu
wa ngozi wilayani kwetu”,alisema Nkurlu.
Kwa
upande wake mlemavu wa ngozi, Hidaya Omari,ametumia nafasi hiyo kuiomba
serikali ihakikishe wataalam wa masuala ya ualibino,wanapatikana kwa
karibu zaidi.Kitendo hicho kitasaidia kubaini mapema dalili za kansa ya
ngozi.
Kwa
mujibu wa Afisa mahusiano wa Chama Cha Walemavu wa ngozi Tanzania,
Josephat Tona,watu wenye ualibino asilimia 80 ambao wengi wao wanaishi
miaka 32,hufariki dunia majumbani kutokana na kukosa wataalam wa masuala
ya walemavu hao.
Mkoa
wa Singida wenye wilaya sita, una daktari moja tu ambaye hata hivyo
hana usafiri wa kumwezesha kuwafikia walemavu wa aina mbalimbali
wakiwemo na wa ngozi.
Chanzo: Dewjiblog
Sign up here with your email