Mwanasiasa Mkongwe katika siasa za Tanzania mzee Kingunge, jana katika hali isiyotarajiwa alijiunga na kuzungumza dakika 40 katika kampeni za CHADEMA jijini Arusha katika viwanja vya Unga Limited na kutoa dhamira yake kwa nini anamuunga mkono mgombea wa uraisi chini ya mwanvuli wa UKAWA kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ndugu Edward Lowassa katika viwanja vya Unga Limited.
Kingunge katika kampeni za chama cha CHADEMA jana jioni
Mzee kingunge kadi namba 8 CCM, na kati ya waanzilishi ishirini wa CCM mwaka 1967, tarehe 4 Oktoba 2015 alitangaza rasmi kwa sababu nyingi alizozieleza kufikia hatua ya kujitoa CCM.
Katika mkutano wa kampeni ya Chadema jijini arusha alisema kuwa yeye ni mtu wa "Mabadiliko na kuwasisitiza wasiogope kufanya mabadiliko". Katika dakika 40 alizozungumza alisema amekuwa akishuhudia vyama mbalimbali katika kampeni za mwaka huu lakini UKAWA wametia fola. Hakuishia hapo alisema
Mimi nimekuwa nikimuunga mkono Lowassa hata kabla hajatoka ndani ya CCM
Mzee kingunge bado alikaza kwa kusema hajahamia chama chochote cha kisiasa na kwamba yeye ni miongoni mwa watu wanao amini kuhusu mabadiliko.
Baadaye Mheshimiwa Lowassa alimsifu mzee kingunge kwa kusema kwa miaka mingi sasa kingunge amekuwa nguzo ya chama cha Mapinduzi CCM, na alimfahamu kama mtu aliyependa kusimamia maamuzi yake siku zoote.
Baada ya kumaliza mkutano Mzee Kingunge alimshukuru na kumpongeza ndugu Edward lowassa na kumtia moyo katika siku zilizobakia kwa kampeni zake.
Bonyeza hapa kutazama video fupi hapa: KINGUNGE
Sign up here with your email