![]() |
| Dk. John Magufuli |
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, amesema
Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC), limemrahisishia kazi ya kutoa
fedha kwa Tanzania ya kusambaza umeme, hivyo hakutakuwa na ugumu katika
usambazaji umeme.
Dk Magufuli mwenye historia ya kusimamia utekelezaji wa miradi ya
maendeleo katika sekta ya barabara nchi nzima, alisema hayo jana kwenye
mkutano wa kampeni, aliofanya mjini Bahi mkoani Dodoma. Kauli hiyo ya Dk Magufuli na nyingine ambazo amekuwa akitoa katika
kampeni zake, zinazoingia katika mkoa wa Singida ambao ni wa 17 sasa,
zimeonesha tofauti ya ahadi anazotoa kwa wananchi na zile zinazotolewa
na mgombea wa urais wa Chadema, aliye chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward
Lowassa.
Tofauti kubwa imejionesha katika ahadi za Dk Magufuli, kwa kutambua
na kuahidi kudumisha na kuendeleza kazi zilizofanywa na viongozi wa
awamu zilizomtangulia na zinazoendelea kufanyika katika Awamu ya Nne
inayoishia ukingoni.
Kwa upande wa Lowassa, yeye na wapigadebe wake wamekuwa wakionesha
kwamba hakuna kilichofanyika katika miaka 54 iliyopita tangu nchi
ilipopata Uhuru, wala kinachofanyika katika uongozi wa sasa.
Hata katika umeme, hawasemi kuwa kwa sasa Watanzania wanaopata
nishati hiyo ni asilimia 46 kutoka asilimia 10 ya mwaka 2005, kutokana
na jitihada za Serikali kwa kutumia fedha za ndani na nje, ambazo sasa
zimeongezewa nguvu na fedha za MCC
Sign up here with your email
