Charles Boniface Mkwasa amepewa
mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu
na kumalizika Machi 31, 2017.
TFF Imefikia makubaliano hayo na
kocha Mkwasa baada ya kurudhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi
cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare
ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.
Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.
Naye kocha Mkwassa ameeleza
kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada
kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda. Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.
Sign up here with your email