![]() |
| Saratani |
Utafiti wa kampuni moja ya Sweden
uliofanyiwa watu milioni 5 umeonekana kuthibitisha nadharia kwamba urefu
wa mtu na hatari za ugonjwa wa saratani zina uhusiano. Utafiti
huo umebaini kwamba watu warefu wana hatari ya kushikwa na saratani ya
matiti pamoja na ile ya gozi miongoni kwa magonjwa kadhaa ya saratani.
Matokeo
yake yalibaini kwamba kwa kila ziada ya sentimita 10,wakati mtu
anapokuwa mtu mzima hatari za kushikwa na saratani huongezeka kwa
asilimia 18 miongoni mwa wanawake na asilimia 11 miongoni mwa wanaume.
Lakini wataalam walisema kuwa utafiti huo haukuangazia hatari nyingine ambazo watu warefu hawafai kuwa na wasiwasi nazo.
Tafiti
za awali zimeonyesha uhusiano kati ya urefu wa mwanadamu na hatari za
kushikwa na ugonjwa wa saratani,ijapokuwa haijulikani ni kwa nini.
Ripoti
za awali za utafiti huo zilizowasilishwa katika mkutano wa wagonjwa wa
watoto,watafiti kutoka taasisi ya Karolinska mjini Stockholm walielezea
vile walivyolifuatilia kundi moja la watu wazima kwa zaidi ya miaka 50.
Wanawake warefu wana hatari kubwa ya hadi asilimia 20 ya kupatikana na
saratani ya matiti huku wanaume na wanawake warefu wakiwa na hatari ya
juu ya kupatikana na saratani ya ngozi kwa asilimia 30.
Sign up here with your email
