Sepp Blatter na Michel Platini wawajibishwa na FIFA


Kamati ya maadili katika shirikisho la soka duniani FIFA imependekeza Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA asimamishwe kazi kwa siku tisaini kwa tuhuma za Rushwa juu ya matumizi mabaya ya fedha za FIFA.

Wanachama wa kamati hiyo walikutana wiki hii baada ya Jaji mkuu nchini Uswizi kufungua mashtaka ya uhalifu dhidi ya Blatter mwezi uliopita.


Blatter anatuhumiwa kwa kutia saini kandarasi zisizo na manufaa yoyote kwa FIFA mbali na kufanya 'malipo' kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini.

Blatter ambaye ni raia wa Uswizi amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka 1998 na Platini ambaye anataka kumrithi amekana madai yoyote ya kufanya uovu. Hakuna uamuzi ulioafikiwa kuhusu kumchukulia hatua yoyote Platini.

Chanzo: DailyMail
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com