Waziri wa fedha Saada Mkuya Salum
SHIRIKA la Fedha Duniani (IMF) limesema kuwa limevutiwa na kukua kwa
uchumi wa Tanzania.
Limesema uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 na utaendelea kukua kwa kiwango hicho katika miezi iliyobakia mwaka huu hadi mwakani.
Limesema uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 na utaendelea kukua kwa kiwango hicho katika miezi iliyobakia mwaka huu hadi mwakani.
Hayo yamo katika taarifa ya Ujumbe wa IMF, uliotembelea Tanzania
kuanzia Septemba 17 hadi Septemba 30 mwaka huu. Ujumbe huo ulioongozwa
na Herve Joy na ulikuja kufanya mapitio ya uchumi wa Tanzania.
“Pato la Taifa lilitarajiwa kukua kwa asilima 6.5 katika robo ya
kwanza ya mwaka huu na ongezeko kubwa katika uchumi lilitoka katika
huduma za usafirishaji, uzalishaji wa umeme, teknolojia ya habari na
mawasiliano na huduma za fedha,” ilisema taarifa hiyo. Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema katika hotuba yake ya
Bajeti ya Serikali mwezi Juni mwaka huu kwamba uchumi utakua kwa
asilimia 7 mwaka huu na asilimia 7.3 mwaka ujao.
Ujumbe huo wa IMF pia ulisema mfumko wa bei wa Tanzania, ulipanda
kidogo katika miezi michache iliyopita hadi kufikia asilimia 6.4 mwezi
Agosti mwaka huu, na sababu kubwa ilikuwa ni ongezeko la bei ya vyakula
na kushuka kwa viwango vya ubadilishanaji wa fedha. Ujumbe huo uliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua
madhubuti za kuinua na kuboresha uchumi, ikiwemo kuweka sera nzuri za
fedha na kuongeza mazao yanayouzwa nje ya nchi, hatua ambazo pia
ziliimarisha Shilingi.
Hatua hizo pamoja na nyinginezo, ziliboresha masoko ya ubadilishaji
wa fedha za kigeni na biashara kati ya benki mbalimbali. Kwa sasa
Shilingi ya Tanzania inakaribia kurejea katika hali yake ya kawaida,
ilieleza taarifa hiyo ya IMF. Hata hivyo, ujumbe huo wa IMF ulieleza kuwa serikali haikufanikiwa
kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yake ya hadi mwezi Juni mwaka huu ya
ukusanyaji wa mapato.
Sign up here with your email
