YATOSHA NIGHT

Ofisa Uhusiano wa airtel Jane Matinde.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imezindua huduma nyingine ya ‘Yatosha’ itakayowezesha wateja wake kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi bila kikomo kwa kiwango cha Sh 300.
Aidha huduma hiyo pia inaambatana na kifurushi cha intaneti cha MB 10. Huduma hiyo inaitwa “Yatosha Nyts” inawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kupiga simu Airtel kwenda Airtel na kutuma ujumbe mfupi kwenda mitandao yote kila siku kuanzia saa 5:00 usiku hadi saa 12:00 asubuhi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema ‘Yatosha Nyts’ ni ofa kabambe na ya kipekee inayokidhi mahitaji ya wateja wao. “Tumezindua “Yatosha Nyts” ofa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu ya kuwasiliana na kupanga shughuli za siku inayofuata bila hofu ya kupungukiwa na salio kwenye simu zao. “ alisema Matinde.
Kujiunga na “Yatosha Nyts” mteja anatakiwa kupiga *149*99#.
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com