Meneja Kitengo cha Airtel Money Asupya nalingigwa.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel jana imetangaza kugawa zaidi ya
Sh bilioni tano kwa wateja na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel
Money nchi nzima. Uamuzi huo wa kutoa gawio katika akaunti ya udhamini
ya wateja wa Airtel Money litawawezesha wateja wa Airtel kulipwa kiwango
kizuri cha gawio la faida.
Kiwango hiki cha pesa kitalipwa kutokana na kiasi cha pesa mteja
alichokuwa nacho kwenye akaunti yake ya Airtel Money kila mwisho wa siku
kuanzia Machi 2014 hadi Aprili 2015. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa kitengo cha Airtel
Money, Asupya Nalingigwa, alisema wanayo furaha kutangaza mgawanyo huo
wa gawio la faida kwa wateja wao baada ya Benki Kuu ya Tanzania
kuidhinisha kutoa pesa hizo katika akaunti ya udhamini ya pesa za wateja
wa Airtel Money.
Alisema wateja wa Airtel Money watapata sehemu ya gawio lao kulingana
na salio wanalokuwa nalo kwenye akaunti zao kila siku. Airtel imekuwa
mstari wa mbele katika kutoa huduma za kibunifu za kifedha kupitia simu
za mkononi ikwemo NFC huduma inayokuwezesha kufanya malipo kupitia kadi,
Mikopo ya Timiza na huduma nyingine nyingi.
Sign up here with your email