![]() |
| Jose Mourinho |
MASHABIKI wa klabu ya Chelsea wamemtupia lawama
kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, baada ya kumuweka benchi beki wake, John Terry katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Porto.
kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, baada ya kumuweka benchi beki wake, John Terry katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Porto.
Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Dragao nchini Ureno,
Chelsea ilikubali kichapo cha mabao 2-1, huku beki wake akiachwa benchi
na kocha huyo.
Kitendo hicho kiliwafanya mashabiki watume ujumbe mbalimbali katika
klabu hiyo wa kudai kwamba wanamtaka beki huyo kupewa nafasi ya kuanza
kama ilivyo mwanzo.
Hata hivyo, wakati mchezo huo unaendelea baadhi ya mashabiki
walionekana wakiwa na mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yanasomeka
‘tunamtaka nahodha wetu katika kikosi’.
Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand, baada ya
kumalizika kwa mchezo huo aliongea kupitia kitua cha utangazaji nchini
England na kusema kuwa kikosi hicho kilikosa mchezaji ambaye ni kiongozi
kama Terry na kilikosa umoja na ushirikiano.
Terry amekuwa na mchango mkubwa katika klabu hiyo kwa miaka mingi,
lakini kwa sasa kocha huyo ameanza kumuacha benchi katika baadhi ya
michezo, huku Chelsea ikiwa inapoteza michezo hiyo.
Sign up here with your email
