![]() |
| Cristiano Ronaldo |
NYOTA
wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo,
amefanikiwa kufikisha mabao 500 katika historia yake ya soka baada ya juzi kuifungia klabu yake mabao mawili katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Malmo. Mabao hayo ya Ronaldo yametokana na kucheza michezo 753 katika klabu mbalimbali pamoja na timu yake ya taifa ya Ureno.
amefanikiwa kufikisha mabao 500 katika historia yake ya soka baada ya juzi kuifungia klabu yake mabao mawili katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Malmo. Mabao hayo ya Ronaldo yametokana na kucheza michezo 753 katika klabu mbalimbali pamoja na timu yake ya taifa ya Ureno.
Hata
hivyo, amekuwa ni mchezaji ambaye anaongoza kwa mabao mengi katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa, huku akiwa na jumla ya mabao 82, akimuacha
mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, mabao matano ambaye ana mabao
77.
Baada
ya kufikisha mabao hayo, Ronaldo amefanikiwa kuongea na vyombo vya
habari kwa mara ya kwanza tangu miezi tano iliyopita kutokana na
kushambuliwa na waandishi wa habari, lakini baada ya mchezo wa juzi
alifanikiwa kuongea.
“Ni
furaha kuisaidia timu yangu kufanya vizuri, ninaamini nitaendelea
kufanya hivyo kwa kuwa bado nina nafasi, nilikuwa kimya sana kuongea na
vyombo vya habari kutokana na maswali yao yanakuwa si mazuri, wanaweza
kukuuliza swali kutokana na tukio ambalo lilifanyika miezi sita
iliyopita,” alisema Ronaldo.
Hata
hivyo, kutokana na mabao hayo, Ronaldo ameifikia rekodi ambayo iliwekwa
na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Raul Gonzalez, ambaye alipachika
mabao 323 akiwa na klabu hiyo baada ya kucheza michezo 741 kuanzia mwaka
1994 hadi 2010, huku Ronaldo akicheza michezo 308 na kuifikia rekodi
hiyo.
“Furaha
nyingine ambayo ninayo ni kuifikia rekodi ambayo iliwekwa na Raul,
lakini kitu muhimu zaidi ni kuibuka na ushindi na klabu yangu kwa kuwa
mchezo ulikuwa mgumu,” aliongeza Ronaldo.
Ronaldo,
mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na klabu ya Real Madrid mwaka 2009,
akitokea Manchester United na amefanikiwa kuchukua uchezaji bora wa
dunia wa Ballon d’Or msimu uliopita.
Sign up here with your email
