Waziri Simbachawene: Tatizo la Umeme ni la Muda mfupi..!!!

 Waziri wa Nishati na Madidi George Simbachawene
 
SERIKALI imesema tatizo la kukatika kwa umeme ni la muda mfupi na kwamba linafanyiwa kazi kupata ufumbuzi wa kudumu. Aidha, imesema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na kupungua kwa uzalishaji umeme katika bwawa la Mtera, ambalo kutokana na kukabiliwa na ukame, huenda mitambo yake ikazimwa.

Kutokana na hali hiyo, nguvu kubwa kwa sasa inaelekezwa katika umeme wa gesi, huku tatizo la kukatika kwa umeme linatarajiwa kwisha ifikapo Oktoba 20, mwaka huu baada ya mitambo yote inayozalisha umeme kwa kutumia gesi, kuwashwa na kuingizwa katika gridi ya Taifa zaidi ya megawati 870.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene katika mkutano wake na waandishi wa habari jana.

“Mtera tunakusudia kuzima mitambo kwani hakuna maji, ” alisema.
Alisema katika bwawa la Kidatu ambalo limekuwa likizalisha megawati 204 sasa linazalisha megawati 27, na bwawa la Mtera ambalo lilikuwa likizalisha megawati 80, sasa linazalisha megawati tisa.

Bwawa la Kihansi ambalo lilikuwa likizalisha megawati 180, sasa linazalisha megawati 45, na bwawa la Pangani ambalo lilikuwa likizalisha megawati 80, sasa linazalisha megawati 25.

Simbachawene alisema mabwawa hayo, yaliyokuwa yakizalisha megawati 561.5 sasa yanazalisha megawati 105 tu. Alisema umeme unaotegemewa ni ule wa gesi, ambapo mpaka sasa mitambo iliyowashwa imefanikiwa kuzalisha megawati 135.

Alisema upungufu wa megawati 200, ndio unasumbua sasa, kwani tayari wamefanikiwa kuwasha mitambo minne ambayo imetoa megawati 135 za umeme. “Uhakika wangu ni kuwa ifikapo Oktoba 20, mwaka huu mitambo yote iliyokusudiwa iwe imewaka,” alisema.

Waziri huyo alisema Watanzania wamekuwa hawaelewi kwa nini umeme wa gesi umekuwa ukichelewa, kwani gesi kufika ni jambo moja na mitambo kuwashwa ni jambo lingine. ”Mitambo ya Tegeta iligoma kuwaka mpaka wakaitwa wataalmu kutoka nje ya nchi na sasa hali ya umemne imeanza kutengemaa katika Jiji la Dar es Salaam,” alisema.

“Watanzania watuvumilie, tatizo hilo litaisha baada ya mitambo yote kuwashwa, kwani mitambo hiyo haiwashwi tu, lazima ifanyiwe majaribio ndipo iwashwe,” alisema.

Alisema kinachosumbua ni kuwasha mtambo mmoja mmoja. Alisema umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta mazito, umekuwa na gharama kubwa ambayo serikali haiwezi kuimudu.
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com