Mtuhumiwa wa makosa ya mtandao Benedict Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza kulia) anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akisubiri kusomewa mashitaka.
Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud
and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika
Kusini (wa pili kulia), Huang Kun Bing (26) Raia wa China (wa tatu
kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza kushoto) Hefeez Irfan (32) (wa
pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig (41) (wa tatu kushoto) wote watatu
raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu
wakisubiri kusomewa mashitaka ya wizi kwa kutumia mitandao ya simu
(fraud and use of telecommunication network).
Sheria mitandao imechukua sura mpya ilikudhibiti masuala ya matumizi mauri ya mtandao kwa kila mtumiaji ikiwa ni pamoja na kupambana na usambazaji wa taarifa zenye uchochezi, taarifa za kubuni na kusababisha mitafaruku katika jamii.
Kwa hivi sasa matumizi ya kimtandao yameongezeka kwa kasi kubwa hii ni kwasababu ya ugunduzi wa vyombo vya kisasa katika kupata mtandao kama simu za mkononi (smartphones), tablets, computer, Sateliti na vifaa vingine vingi ambavyo ndivyo vinavyotumiaka kautmia mtandao.
Kukua kwa sayansi na teknologia ya mawasiliano nayo ni sababu kubwa ambapo matumizi ya kimatandao yameongezeka kwa kasi. Uhitaji wa jamii kupata upenyo wa kimtandao unafanya kila siku kuwe na namna mopya ya kupata mtandao.
Kwa hivi sasa habari huweza kusambaa ndani ya sekunde moja na kusambaa ulimwengu mzima, kwani kasi ya mtandano ni kubwa sana kwa hivi sasa ikilinganishwa na hapo zamani kwani hata vifaa vingi vya Kitehama havikuwa kwa wingi kama ilivyo sasa.
Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23 na watuhumiwa wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.
Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23 na watuhumiwa wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.
Sign up here with your email