JURGEN NOBERT KLOPP: Meneja mpya Liverpool

 Jurgen Nobert Klopp

Liverpool imemteua Jurgen Klopp kuwa meneja wake mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.

Klopp raia wa Ujerumani mwenye miaka 48 anachukua nafasi ya Brendan Rodgers aliyetimuliwa hivi karibuni baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa miaka mitatu na nusu.

Jurgen Nobert Klopp ni raia wa Ujerumani ambaye ni kocha na mchezaji mpira wa miguu wa zamani Ujermani. Kwa hivi sasa ndie kocha mpya mteule katika timu ya mpira wa miguu ya Uingereza ya Liverpool.

WASIFU WA JURGEN KLOPP:
  • Jina Kamili: Jurgen Nobert Klopp
  • Alizaliwa: Juni, 16 1967
  • Kimo (Urefu): Mita 1.93
  • Ameoa: Ndiyo
  • Watoto: Marc Klopp
  • Jina la Mke wake: Ulla Sandrock (2005)
  • Timu alizofundisha: Liverpool F.C (Tangu 2015), Borussia Dortmund(Tangu  2008-2015).
  •  Tuzo mbalimbali: Kocha bora wa Mwaka Ujerumani, Deutscher Fernsehpreis - Program bora wa Michezo.
 Jurgen Klopp akiwa na Mke wake Ulla Sandrock

Klopp amekuwa nje ya dimba tokea mwezi Mei mwaka huu baada ya kudumu na klabu ya Borussia Dortmund kwa misimu saba.

Anatarajiwa kuanza kazi kwenye klabu hiyo ya Liverpool na wasaidizi wake Zeljko Buvac na Peter Krawietz aliofanya nao kazi akiwa kwenye Ligi ya Bundesliga.

Klopp anatarajiwa kutambulishwa rasmi na klabu yake mpya siku ya Ijumaa katika mkutano na waandishi wa habari.

Alijiunga Dortmund mwaka 2008 na kuiongoza kushinda vikombe viwili vya ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga).
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com