AJARI: Loli lapinduka na kuua mtu mmoja


Mtu mmoja amepoteza maisha papo hapo baada ya gari alilokua akitembelea Corola Primio lenye nambanza usajili T 444 CST kuangukiwa na Lori aina ya Scania T 424AEB lililo beba Kontena na kuvutwa na tela lenye namba za usajili T 653ABW ambalo lilipinduka hii leo mchana katika eneo la Temeke Vetenary jirani na soko barabara kuu ya Mandela, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Mtu mmoja mwanamke alinusurika katika ajali hiyo baada ya kutoka salama na kutoweka

Wananchi wakiwa wamekusanyika wakiangalia uokoaji kutoka kwa kikosibcha zimamoto cha jiji la Dar es Salaam wakisaidiana na wananchi.


Gari hilo dogo likiwa limeharibika vibaya baada ya kuangukiwa na tera la lori hilo la mizigo likisogezwa tayari kwa kukatwa na kutoa mwili wa marehemu. 


Askari Polisi wa usalama barabarani wakitoa maelekezo ya jinsi ya uvutaji wa gari ndogo iliyoangukiwa na tera la Lori la mizigo


Gari ndogo ikivutwa katika sehemu nzuri na gari ya kuinulia mizigo chini ya polisi wa usalama barabarani waliofikwa muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea.  
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com