KAYUMBA JUMA: MSHINDI WA BSS AWAMU YA NANE 2015


Baada ya kazi nzito katika mchakato mzima wa BSS, Finali zimesha malizika usiku huu na akapatikana mshindi katika awamu ya nane ya BSS ambaye ni KAYUMBA JUMA, kijana mwenye umri wa miaka 19 Mkazi wa Dar es salaam na alishiriki kama muwakilishi wa Dar es salaam.


Madam Rita akitangaza Msindi wa BSS 2015

 Kayumba Juma (19) akiwa anashangilia baada ya kutangazwa Mshindi






 Kayumba akimshukuru Mungu kwa kumfanya Mshindi wa BSS 2015



Kayumba akiwa amekabidhiwa Briefcase ya Bongo star search kama Mshindi
 Kayumba Juma BSS 166 (Kabla ya Finali)

Kayumba Juma BSS 116 akiwa jukwaani

Kazi hii ngumu ilifanywa na majaji watatu katika siku hii ya fainali Akiwepo Master Jay, Salama Jabir na jaji Mkuu Rita Paulsen (Madam Rita).



                                                 Rita Paulsen (Madam Rita)



Salama Jabir (Jaji)


 Joachim Kimaryo a.k.a Master Jay
 
Mshindi amejipatia Milioni 60 ambapo Mil 50 ni ya kwake na Mil 10 ni sehemu ya usimamizi wa muziki kutoka kwa wasimamizi wa Tip Top Connection wanaosimamia muziki wa Diamond Platnumz, Yamoto Band, Madee n.k. Mbali na zawadi hiyo ya hela, pia mshindi amepata simu ya Huawei P8 kutoka kwa wadhamini wetu wa HUAWEI huku wengine wakipata Huawei Light.

Kayumba Juma alionyesha umahiri wake mkubwa katika usiku huu ambapo aliimba nyimbo kwa uzuri mpaka kupelekea mashabiki kumtaja kabla ya Jaji mkuu kumtaja mshindi wa Kwanza wa BSS mwaka 2015. Kayumba akiwa katika tatu bora zaidi aliimba wimbo wa Yamoto Band na akamalizia wimbo wa Nani kama mama wa Aisha Mashauzi, ambao ulifanya avute mashabiki mbele ya ukumbi na kumfanyia shangwe nyingi huku akiendelea kuimba mbele.

Kayumba Juma aliimba kwa ustadi mkubwa nyimbo zake zote kiasi kwamba unaweza kudhani nyimbo hizo ameimbaayeye mewnyewe.

 Kayumba Juma akiwa katika Jukwaa kabla ya kufika Fainali

Top six wakiwa Ukumbini kwa ajili ya kuanza kuonyesha vipaji katika fainali hizo.






Photo Credits: Andrew Chale, modewjiblog
Kwa ajili ya Habari nyingine kuhusu BSS bonyeza hapa: BSS 2015
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com