Bodi ya parole jijini Johannesburg, Afrika Kusini ilitarajiwa kutoa uamuzi wa kama itamwachia huru Oscar Pistorius kutoka gerezeni Jumatatu hii.
Bodi hiyo ilikutana jijini Durban mwezi uliopita lakini iliahirisha kesi yake kwa wiki mbili.Katika kipindi hicho idara ya haki ilisema haikupata muda wa kumaliza kesi ya Pistorius kutokana na kuwa na mambo ya kuyapitia.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mkutano wa Jumatatu hii utafanyika Johannesburg.
Mwanariadha huyo mlemavu alifungwa mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake huko Pretoria kwenye Valentine’s Day, mwaka 2013. Hadi sasa ameshakaa jela kwa mwaka mmoja ambapo awali alikuwa aachiliwe August 21 kuendelea na kifungo cha ndani.
Sign up here with your email