Mwenyekiti wa label ya HKN records inayomsimamia Davido, Adewale Adeleke ambaye pia ni kaka yake ametangaza tarehe mpya ya kuachia album mpya ya star huyo wa Nigeria, ‘Baddest’ baada ya kushidwa kutoka mwezi September kama ilivyopangwa awali.
Mara ya kwanza album hiyo ilipangwa kutoka June 8, 2015, lakini ilisogezwa tena hadi August 8 ambapo napo ilishindikana na kusogezwa hadi September ambayo ilipita kimya kimya mpaka sasa imepewa tarehe mpya ya October 10.
Album hiyo ambayo imekuwa ikipangwa kuachiwa na kuahirishwa mara tatu, sasa itatoka Jumamosi ya October 10, 2015.
Mastaa mbalimbali wa Marekani akiwemo Meek Mill, Drake, Trey Songz, Akon na wengine ni miongoni mwa wasanii wa kimataifa walioshirikishwa kwenye album hiyo.
Chanzo: Bongo5
Sign up here with your email