Unapozungumzia
tasnia ya filamu nchini basi huwezi kuacha kuzungumzia makampuni ya
kusambaza kazi za filamu Tanzania na Nje ya Tanzania. Kuna Makampuni
mengi sana ambayo yanasambaza kazi za filamu ndani na Nje ya Tanzania
lakini Katika Makampuni hayo huwezi kuacha Kuitaja Kampuni ijulikanayo
kama PROIN PROMOTIONS LTD yenye makao yake Mikocheni na Mabibo.
Proin
Promotions Ltd ni kampuni ya kutengeneza na kusambaza filamu za
Kitanzania ndani na nje ya Tanzania ambapo Mwaka huu mwezi Agasti 30
ilitimiza Miaka mitatu tokea kuanzishwa Kwake na kuzinduliwa rasmi siku
hiyo ya Agasti 31 2013 katika Ukumbi wa Mlimani City Unaweza kujiona HAPA jinsi
uzinduzi ulivyokuwa huku siku hiyo ya Uzinduzi wa Kampuni hii ukienda
Sambamba na Uzinduzi wa Filamu ya Msanii Elizabeth Michael almaarufu LULU iitwayo Foolish Age.
Ni
Kampuni ambayo imeleta Ushindani katika Soko la filamu Tanzania haswa
baada ya kuingia katika soko na kufanikiwa kuliteka soko la filamu
kutokana na aina ya staili iliyoingia nayo kwenye soko la filamu. Ndani
ya Mwaka mmoja Proin iliweza kutikisa katika soko la filamu kwa kuleta
mabadiliko ambayo kiukweli yameweza kuonekana katika Tasnia hii ya
Filamu nchini.
Kuingia
sokoni na Staili ya kuuza Filamu iliyo na Sehemu Moja (Part 1tu) na
Kutonunua hakimiliki za wasanii ni moja ya vigezo vilivyoipandisha Hadhi
kampuni hii ya Kizalendo ambayo imelenga Kukuza na kunyanyua Tasnia ya
Filamu nchini.
Leo hii unapozungumzia Swala la Filamu za Kitanzania hutoweza kuacha kutaja Kampuni ya Proin kutokana
na Umahiri wake katika kutengeneza na kusambaza filamu na Ubora wa Kazi
zake ambazo nyingi zimeweza Kuchukua tuzo Nchini Marekani huku Filamu
yake Ya Kigodoro ikiwa mojawapo kati ya filamu nyingi za Proin zilizofanya Vizuri katika Soko la Filamu Nchini ukiachilia mbali Mapenzi ya Mungu, Family Curse, Never Give Up, Kutakapokucha, Mpango Mbaya, na ambayo imeingia Hivi karibuni Sokoni iitwayo Mwanaharusi Unapozungumzia
Kantangaze” neno ambalo limechukua nafasi kubwa sana katika jamii ya
Kitanzania sahivi basi hutoacha kuitaja Filamu ya “KIGODORO KANTAGAZE” ambayo ndipo neno hilo lilipotoka.
Proin
Promotions imetoa takribani Filamu 25 tokea kuanzishwa kwake huku
filamu zote zikiwa na viwango vya uhakika ambavyo zinaweza kuangaliwa na
rika lolote lile huku ikijivunia Ubora wa Picha, Sauti na hata stori za
filamu hizo.
Achilia
mbali Kusambaza Filamu tu Proin Promotions ilikuja na Kitu ambacho
mpaka leo kimeifanya Kampuni ya Proin Promotions Ltd kuwa juu kutokana
na Uthubutu wake katika kuzunguka Mikoani kutafuta Vipaji vya vijana
wenye uwezo wa kuigiza lakini hawakupata nafasi ya Kuonekana na mradi
huo ujulikanao kama Tanzania Movie Talents (TMT)
Tanzania
Movie Talents ni Shindano la Kuibua na kusaka Vipaji vya Kuigiza Nchini
ambapo vipindi vyake vilikua vikirushwa kupitia Kituo cha Runinga cha
ITV ambapo vijana wengi waliweza kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao
huku washindi wa shindano hilo katika Mikoa walikua wakiondoka na Kitita
cha Shilingi laki Tano huku mshindi wa Kwanza katika fainali hiyo
akiibuka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania. Shindano hilo
kwa mara ya kwanza lilianza kufanyika Mwaka 2014 huku mshindi wa Kwanza katika fainali ya TMT 2014 iliyofanyika Mlimani City tarehe 30 Agasti 2014 kutoka Mtwara Mwanaafa Mwinzago Kuibuka Mshindi
Shindano
la TMT limeweza kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu kutokana na
kuzalisha vipaji na sura mpya katika tasnia ya filamu huku Ikiwa na Zao
la Filamu Moja yenye viwango vya kimataifa iitwayo “Mpango Mbaya” Filamu
hii ilitengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd huku ikichezwa na
washiriki wa Shindano la TMT 2014 na kutoa nafasi kwa washiriki
kujipatia kipato kutokana na utengenezaji wa filamu hiyo pamoja na mauzo
ya filamu hiyo.
Proin
Promotions Ltd Imeweza kuleta Changamoto katika tasnia ya filamu
kutokana na kuzalisha vipaji na sura mpya katika tasnia hiyo huku
washiriki wa TMT wakianza kuonekana katika baadhi ya Filamu za wasanii
wengine kutokana na Kushiriki kwao katika filamu nyingine na baadhi ya
Matangazo Lengo Moja wapo la Kampuni ya Proin Promotions Ltd limeweza
kutimia na kuthibitika kutoka na kutoa nafasi kwa wasanii wachanga
kuonekana na kuanza kufanya kazi ambapo zimeanza kuingia katika Soko la
Filamu nchini.
Moja
ya zao la Washiriki wa TMT ni filamu iitwayo Mpango Mbaya kama hujaweza
kupata Nafasi ya Kuiangalia unaweza kununua nakala yako halisi na
kujionea ubora wa kazi hiyo kuanzia Picha, Stori na Sauti. Vilevile
wapenzi wa TMT wajiandae kukaa mkao wa kula kwa kupokea kazi nyingine
mpya kutoka kwa washiriki wa TMT 2015 huku ikitarajiwa kuwa Ni nzuri
zaidi ya washiriki wa Mwaka jana.
Kwa
mantiki hiyo Kampuni ya Proin Promotions imeweza kuwa moja ya Kampuni
mahiri katika Utengenezaji wa Filamu na Bidhaa za filamu nchini
Tanzania.
Proin
Promotions ltd iliweza kuhudhuria Maonyesho mbalimbali ya Kimataifa
Nchini Kenya na kuweza kuliteka pia Soko la Filamu Nchini Kenya huku
ikijipatia Mwanya wa kufanya kazi na wasanii wa Kenya. Na hii ndio Proin
Promotions Ltd yenye Kumuongoza na Kumsimamia Kikazi Msanii Elizabeth
Michael almaarufu Lulu.
Makala nyingine itakujia hivi karibuni: Dewjiblog
Makala nyingine itakujia hivi karibuni: Dewjiblog
Sign up here with your email