MGOMBEA wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Edward Lowassa amesema kwamba iwapo atapata ridhaa ya wananchi
ya kuchaguliwa kuiongoza nchi ataunda serikali rafiki kwa waendesha
bodaboda nchini ili kutetea na kuboresha maslahi yao.
Akihutubia wananchi wa wilayani Babati, mkoani Manyara juzi alisema
anataka kuona bodaboda wanapata malipo sahihi pamoja na kufanya kazi zao
kwa uhuru ili kuinua kipato chao na kuondokana na umasikini.
“ Naomba mnichague kuwa Rais nina uwezo na nimejiamini kuwa natosha,
ninagombea kwa sababu nimechoka na umasikini, mtu anakula mlo mmoja kwa
siku, ni wakati wa watu kuondokana na umasikini,” alisema.
Alifafanua kuwa kutokana na azma yake hiyo ataongoza taifa kwa spidi
120 kwa saa katika kuleta maendeleo yaliyokusudiwa kwa kuanza na
kipaumbele cha kuboresha elimu ambapo alisisitiza kuwa atafuta ada ya
shule kuanzia elimu ya chekechea hadi chuo kikuu na kuboresha maslahi ya
walimu.
Lowassa alisema anaweka kipaumbele kwenye elimu kwa sababu dunia ya
sasa inaongozwa na teknolojia ya kisasa ambayo ana imani ndio dira ya
kumkomboa Mtanzania wa leo na hasa kizazi kipya.
Aliongeza kuwa endapo atapata ridhaa hiyo atakuwa mtetezi wa wakulima
nchini kwa kuwajengea misingi mizuri ya kupata masoko ya kuuza mazao
yao popote duniani pasipo kutozwa kodi ya aina yoyote
Sign up here with your email
