Magufuli aendelea na kampeni ya 17 mkoani Singida

Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili mjini Itigi mkoani Singida mapema jana mchana,tayari kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni mjini humo. 


 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma (hawapo pichani), alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni.


 Kiongozi wa Msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli,Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt.Magufuli kuwahutubia wananchi wa Ikungi jioni ya jana na kuwaomba kumpigia kura ya ndio ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchahuzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani. 

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida jioni ya jana ,wakati akiwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
 
Dkt. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali  hasa za mashirika ya  dini ambazo zinaendesha hospitali  katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili kuimarisha huduma  za kiafya  kwa jamii.
  
 
Wananchi  wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na pia kuwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.



Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com