TP MAZEMBE YAINGIA FAINALI


Klabu ya TP Mazembe ya Congo DRC, Itakutana na klabu ya Algeria USM Alger katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika.

Mazembe ilijihakikishia nafasi yake siku ya jumapili yaani jana baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merrekh ya Sudan mjini Lubumbashi.

 
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta alifunga mara mbili katika ushindi huo huku Muivarycoast Roger Assale akifunga goli la tatu. Katika mchezo huo wa marejeano TP Mazembe waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 53 ya mchezo kabla ya kuiandikia tena goli la pili katika dakika ya 69. 

Goli la tatu na la mwisho kwa TP Mazembe zidi ya Al-merekh lilifungwa na Assale katika dakika 71. 

Kwa matokeo hayo ya leo Mazembe wanaingia fainali kwa matokeo ya jumala ya goli 4-2, baada ya mchezo wa awali uliochezwa Khartoum Al-merekh waliibuka na ushindi wa goli 2-1, goli la Mazembe katika mchezo huo likifungwa na Thomas Ulimwengu. 

Sasa TP Mazember itacheza dhidi ya USM Alger ya nchini Algeria kati ya oktoba 30 na november 1 mwaka huu ukiwa ni mchezo wakwanza wa fainali ya ligi ya mabingwa Afrika
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com