Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
ameeleza furaha yake baada ya klabu hiyo kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya
mahasimu wao wa jadi Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza
Jumapili.
Wenger amesema alifurahishwa sana na uchezaji wa timu
yake na kueleza kuwa walishangaza Manchester United kuanzia mwanzo wa
mechi.
“Kuanzia kwa Petr Cech hadi kwa Theo Walcott wote walicheza
vyema. Nimenoa timu nyingi kali lakini hakuna hata moja iliyoweza
kucheza mechi 60 katika kiwango sawa. Lazima ukubali kwamba sisi ni
binadamu,” alisema.
“Tuko kwenye kinyang’anyiro (cha kushindania
taji), tuko alama mbili nyuma ya viongozi Manchester City na natumai
matokeo ya leo yatatupa imani ya kuendelea kupigania taji.”
Arsenal
walipata ushindi kupitia mabao mawili ya nyota wa Chile Alexis Sanchez
na Mjerumani Mesut Ozil, mabao yote yakifungwa kipindi cha kwanza kwenye
mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Emirates.
Kwa meneja wa Manchester United Louis Vvan Gaal, ilikuwa vigumu kukubali matokeo hayo. "Tulianza
vibaya sana, bila kuonyesha ari ya kushambulia na kutaka kushinda.
Ilikuwa mara ya kwanza kwangu kushuhudia hilo katika timu yangu.
Sikulitarajia hili,” amesema. "Unapoipatia timu kama Arsenal mianya tele uwanjani ya kusakata gozi, basi unajua kwamba lazima utashindwa.”
Arsenal
na Manchester United sasa zinatoshana alama ingawa Arsenal wako mbele
wakishikilia nambari mbili kwenye jedwali kwa wingi wa mabao. Timu
hizo zitarudi mawindoni wiki mbili zijazo mnamo Oktoba 17, baada ya
mapumziko ya wiki mbili ya mechi za kimataifa, ambako United watakutaka
na Everton uwanjani Goodison Park nao Arsenal wawe ugenini Watford.
Sign up here with your email