Klabu ya soka ya Liverpool ya nchini Uingereza imemfukuza Meneja wake Brendan Rodgers baada ya matokeo mabaya ya muda mrefu.
Uamuzi
wa kumfuta kazi Rodgers ulifanywa hata kabla ya mchezo ulioisha kwa
suluhu dhidi ya Everton ambao uliwaacha Liverpool katika nafasi ya kumi
katika msimamo wa ligi ya England.
''Licha ya kuwa huu umekuwa ni uamuzi mgumu,tunaamini itatupa nguvu zaidi uwanjani,''ilisema taarifa ya klabu.
Meneja
wa zamani wa klabu ya Chelsea na Real Madrid Carlo Ancelotti,kocha wa
Ajax Frank de Boer na meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund
wamehusishwa kujiunga na klabu ya Liverpool katika siku za karibuni
baada ya timu hiyo kuuanza msimu kwa kusua sua.
Chanzo: BBC swahili
Sign up here with your email