Mfahamu Magufuli mgombea urais wa CCM 2015 Tanzania


John Pombe Pombe Joseph Magufuli Mgombea urais kupita CCM kitaaluma ni Mwalimu na mtalaamu wa Kemia aliyezaliwa October 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Kagera Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi huko huko Chato, mkoani Kagera kati ya mwaka 1967 hadi 1975 na baadae kujiunga na chuo cha ualimu Mkwawa kilichopo Iringa kusini mashariki mwa Tanzania kati ya mwaka 1979 na 1982 ambapo alitunukiwa Stahahada ya Ualimu na kuanza kufundisha masomo ya hisabati na kemia katika shule mbali mbali za sekondari kuanzia mwaka 1983.

John Pombe Magufuli hakuishia hapo kielemu kwani aliamua kujendeleza zaidi ambapo alijiunga na chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1985 hadi 1988 ambapo na kutunikiwa shahada ya ualimu katika masomo ya chemia na hisabati ambapo baadae alijikita zaidi katika somo la Kemia kusomea hadi nganzi ya udaktari.

Katika siasa za Tanzania John Pombe Magufuli mwanzoni hakujulikana sana, hadi nyota yake ya kisiasa ilianza kung'aa pale alipogombea na kushinda ubunge mwaka 1995 ambapo mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wizara ya Ujenzi na baadae kupanda ngazi hadi kuwa waziri kamili nafasi aliyonayo hadi hivi sasa.

Wasifu wa nje ya Mshika bendera huyo wa chama cha Mapinduzi CCM katika ngazi ya urais kwa mujibu wa majirani wanaoishi karibu na nyumba yake jijini Dar es Salaam wasema ni anaishi maisha ya kawaida kwani wakati watoto wa baadhi ya viongozi wakisoma shule za hali ya juu watoto wake wamesoma katika shule za kawaida.

Kwa sasa Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndiye mshika bendera ya urais kupitia chama tawala. Hata hivyo tofauti na uchaguzi uliopita mgombea huyo anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hii Edward Lowassa ambaye anagombea kupitia chama cha upinzani cha CHADEMA akiwakilisha muungano usio rasmi wa vyama vinne vya upinzani unaojulikana UKAWA.

Chanzo: BBC Swahili
Previous
Next Post »
Show Comments: OR

Contact us

Name

Email *

Message *

Tangaza nasi

Tangaza nasi
Freebango.com