MGOMBEA urais wa CCM, Dk John
Magufuli amewataka wananchi kumchagua ili awe rais wa tano ajaye wa
Tanzania huku akiahidi kushughulikia masuala mbalimbali ya wananchi na
hivyo kuliletea Taifa maendeleo kwa muda wote atakaokuwepo madarakani.
Akizungumza na wananchi wa
mkoani Lindi katika muendelezo wa kampeni zake, Dk Magufuli alisema
akichaguliwa kushika nafasi hiyo, pamoja na mambo mengine atakayoyafanya
atatumia utajiri wa gesi uliopo katika mikoa ya Kusini, kutoa ruzuku
kwa vifaa vya ujenzi ili kushusha bei na kuwawezesha wananchi kujenga
nyumba bora.
Amesema pia atatumia nafasi
hiyo kutafuta namna bora ya kuwainua wakulima wa korosho, tofauti na
utaratibu wa sasa wa stakabadhi ghalani, alisema umekuwa ukiwasababishia
umasikini mkubwa wakulima wa zao hilo.
Akiwa Nachingwea, Ruangwa,
Mtama na Lindi Mjini, Dk. Magufuli alisema tofauti na wapinzani
wanaoahidi kuondoa nyumba za nyasi na tembe nchi nzima kwa siku 100
watakazokaa Ikulu, jambo alilosema ni ndoto, Serikali yake itakachofanya
ni kushusha bei ya mabati, saruji, nondo, misumali na vifaa vingine vya
ujenzi ili wananchi wajenge nyumba bora.
Akielezea ni vipi atawezesha
hilo kufanikiwa, Dk Magufuli alisema atatumia utajiri wa rasilimali za
Taifa ikiwemo gesi inayopatikanakatika Mikoa ya Kusini na Bagamoyo,
Pwani ili kutoa ruzuku katika vifaa vya ujenzi.
Lakini, pia kuongeza viwanda
vya bidhaa hizo ili kushusha bei kwa kiwango cha juu. Alisema dalili za
kushuka kwa vifaa hivyo, zimeanza kuonekana baada ya kujengwa kwa
Kiwanda cha Saruji cha Dangote mkoani Mtwara, ambachokinatumia nishati
ya gesi kwa uzalishaji, kilichowezesha kushuka kwa bei ya saruji kutoka
Sh 16,000 hadi Sh 8,000 na kwamba bei hiyo itashuka zaidi atakapokuwa
rais.
Alisema pia ataziba mianya yote
ya rushwa serikalini ili makusanyo ya fedha hizo yatumike kuboresha
maisha ya Watanzania wakiwemo wa Kusini, huku akisema ushahidi wa
utendaji wake kwa watu wa Kusini ni ujenzi wa barabara za lami kutoka
Dar es Salaam kwenda Lindi na Mtwara na baadaye Tunduru na Songea.
Ili kumwezesha kuingia Ikulu,
mgombea huyo aliwaomba wakaziwa Mkoa wa Lindi kufika katika vituo vya
kupiga kura mapema asubuhi ya Oktoba25, huku akisema kutokana na vitisho
na vurugu zilizopangwa ili kuwatishia wananchi hasa wanawake wasipige
kura, kutakuwa na polisi wa kutosha ili kulinda amani.
Akizungumzia soko la korosho,
Dk Magufuli alisema akiingia Ikulu atabadili mfumo wa ununuzi wa korosho
ili kuwezesha wakulima wa zao hilo kwa mikoa ya Kusini, kunufaika na
kuboresha maisha yao na kuachana na mfumo wasasa ambao unawafanya
wakulima kukopwa fedha zao bila kulipwa na hivyo kuwa masikini.
Sign up here with your email