KAMPENI za wagombea Ubunge jimbo la Arusha Mjini zimesimama kufuatia
kifo cha Mgombea Ubunge wa chama cha ACT-Wazalendo, Estomiah Mallah
aliyefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC iliyopo wilaya
ya Moshi, Kilimanjaro, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa shinikizo la
damu.
Akithibitisha kupokea taarifa za kifo cha Mgombea
huyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd ambaye pia ni Msimamizi
mkuu wa Uchaguzi katika jimbo hilo, Idd amesema kuwa kampeni ambazo
zitaendelea ni za urais na udiwani, lakini wabunge mpaka tume ya
uchaguzi ipange upya ratiba.
“Kweli mgombea amefariki na nimepata taarifa za kifo hiki leo saa
12:00 asubuhi, toka kwa katibu wa chama chake marehemu ACT-Wazalendo,
Eliamam Motivo,” amesema.
Aidha ametoa pole kwa wafuasi wa chama hicho kwa kuondokewa na mpendwa wao na wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu.
Katibu wa Jimbo la Arusha wa Chama cha ACT-Wazalendo, Eliamam
Motivo amesema amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa mgombea wao
na Mshauri Mkuu wa Chama chao kwa mkoa wa Arusha.
“Mzee alikuwa haumwi lakini kwenye mkutano wa mgombea urais wa
chama chetu Oktoba 6, alipanda jukwaani na baada yakushuka alisema
hajisikii vizuri na kesho yake ambayo Oktoba 7 alikwenda hospitali ya
St. Thomas na alipatiwa matibabu ila hali yake iliendelea kuwa mbaya na
tuliamua kumwamishia hospitali ya KCMC na usiku wa kuamkia leo saa saba
usiku alifariki,” amesema.
Motivo alisema chama hicho kimesimamisha kampeni zote, kwa siku tatu ili kuomboleza msiba huo.
Sign up here with your email