Mgombea urais kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo amesema anaunga
mkono kauli ya mwenyekiti wake wa chama Mh. Augustine Mrema ya ‘kumpigia
debe’ mgombea wa chama cha mapinduzi CCM, Dk John Magufuli, kwa madai
kuwa hayo ni maamuzi yake binafsi.
Mrema akimpamba John Magufuli
Mgombea
urais kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo amesema anaunga mkono kauli
ya mwenyekiti wake wa chama Mh. Augustine Mrema ya ‘kumpigia debe’
mgombea wa chama cha mapinduzi CCM, Dk John Magufuli, kwa madai kuwa
hayo ni maamuzi yake binafsi.
Lyimo amesema kuwa kauli hiyo haijatolewa na mkutano wowote wa chama, bali ni maoni binafsi kwa kuwa mwaka huu watanzania wanachagua mtu na siyo chama na kwamba jambo alilofanya Mrema si jipya wala la ajabu.
“Hili jambo siyo la ajabu, hata Marekani, Colin Powell alitangaza
kumuunga mkono Obama licha ya kuwa chama tofauti, Mrema amesema hivyo
kwa kuwa anajua looser siyo yeye, tumesimamisha wagombea ubunge nchi
nzima, na yeye ni mmoja wapo, kwahiyo hilo halinipi shida” Amesema
Macmillan Lyimo.
Kuhusu mahusiano kati yake na mwenyekiti huyo, Lyimo amesema kuwa mahusiano ndani ya chama hicho ni mazuri na hakuna ugomvi wowote.
“Tunaendelea kushirikiana kama kawaida, na hata kampeni zangu nilianzia kwake na nitafungia jimboni kwake” kauli ya Lyimo Kuhusu nafasi yake ya ushindi, Lyimo amesisitiza kuwa yeye ndiye atakayeshinda urais mwaka huu, na kamwe Rais hatoki CCM.
“Magufuli hawezi kushinda, nafasi kubwa ya ushindi ninayo mimi, hata Magufuli anajua kuwa mimi napinga huo mwenge kwenye picha yake, hiyo ni ishara ya uchawi, na uchawi wake utashindwa mwaka huu”. Amesema mgombea huyo.
Lyimo amesema kuwa kauli hiyo haijatolewa na mkutano wowote wa chama, bali ni maoni binafsi kwa kuwa mwaka huu watanzania wanachagua mtu na siyo chama na kwamba jambo alilofanya Mrema si jipya wala la ajabu.
Macmillan Lyimo, Mgombea Urais kwa tiketi ya TLP
Kuhusu mahusiano kati yake na mwenyekiti huyo, Lyimo amesema kuwa mahusiano ndani ya chama hicho ni mazuri na hakuna ugomvi wowote.
“Tunaendelea kushirikiana kama kawaida, na hata kampeni zangu nilianzia kwake na nitafungia jimboni kwake” kauli ya Lyimo Kuhusu nafasi yake ya ushindi, Lyimo amesisitiza kuwa yeye ndiye atakayeshinda urais mwaka huu, na kamwe Rais hatoki CCM.
“Magufuli hawezi kushinda, nafasi kubwa ya ushindi ninayo mimi, hata Magufuli anajua kuwa mimi napinga huo mwenge kwenye picha yake, hiyo ni ishara ya uchawi, na uchawi wake utashindwa mwaka huu”. Amesema mgombea huyo.
Sign up here with your email