Kwa karne nyingi mmea wa nyanya ulimea katika maeneo ya Andes kwenye
Bara la Amerika ya Kusini lakini wenyeji wa huko, Wahindi Wekundu
hawakuupanda.
Mmea huo ukapelekwa Mexico, wenyeji wa huko, Waaziteki wakaupa jina
la “Xitomati” yaani “Tomati” kubwa. Neno tomati lilitumiwa kwa ajili ya
matunda yanayofanana na nyanya hasa yenye majimaji mengi. Waaziteki
wakaanza kuzitumia nyanya katika mapishi na hatimaye mmea huo ukaanza
kujulikana ulimwenguni kote. Mwaka 1590, Kasisi wa Kikatoliki wa shirika
la Jeisut aliyeishi nchini Mexico kwa miaka mingi, akalisifu tunda la
nyanya na kusema kuwa lina lishe bora na virutubisho na pia tunda lenye
maji mengi linalofanya mchuzi uwe na ladha nzuri.
Jamii ya Wahispania wanaoishi Mexico wanatumia mbegu za mmea huo
nchini kwao na kwenye makoloni yao Ufilipino na nchi za Karrebian .
Licha ya jitihada hizo ilichukua zaidi ya karne tatu kabla ya nyanya
kuanza kutumiwa katika mapishi ulimwenguni kote. Licha ya sifa ya nyanya
nchini Mexico, wananchi Ulaya hawakuzipenda. Tatizo linaanza wakati
wataalamu wa mimea barani Ulaya wanasema wanapozitaja nyanya katika
jamii ya “Solanaceae” yaani wanaulinganisha na mmea uitwao Mbeladona
wenye sumu.
Majani ya Mbeladona yanatoa harufu mbaya na yana sumu. Waganga
wanaotumia miti shamba wanadai kuwa tunda la nyanya lina nguvu ya
kuamsha tamaa ya ngono. Inadaiwa kwamba, sifa hiyo imesababisha watu
waamini kwamba hiyo ndiyo sababu Wafaransa wanaliita tunda hilo “Pomme
de” Amour, yaani “tofaa la mapenzi”. Maoni yasiyofaa kuhusu nyanya
yalienea hadi Amerika Kaskazini.
Mwishoni mwa miaka ya 1820, mkulima mmoja Mmarekani kutoka jimbo la
Masschusetts alisema hivi kuhusu nyanya: Nyanya zilionekana zenye
kuchukiza sana. Katika karne ya 16 Waitaliano wanaliita tunda hilo
Pomodoro, yaani “ tofaa la dhahabu”. Kufikia mwanzoni mwa karne ya 17
nyanya zilianza kuliwa nchini Italia ambako zinastawi vizuri hasa wakati
wa majira ya joto. Inasemekana kwamba nyanya zimepewa jina la tofaa la
dhahabu kwa sababu aina za mwanzo kupandwa na Waitaliano zilikuwa na
rangi ya njano.
Kwa takribani karne mbili, wakulima Kaskazini ya Ulaya wanaendelea
kuutilia shaka mmea huo na tunda lake, na hivyo wanazipanda kwa ajili ya
kurembesha bustani au kwa matibabu. Hadi kufikia miaka ya 1870, nyanya
zilisafirishwa kwa reli kutoka Calfornia na kuuzwa New York nchini
Marekani. Miaka michache kabla ya wakati huo, ilianzishwa sehemu ya
kutengenezea Piza Naples nchini Italia, hivyo kukawa na mahitaji makubwa
ya nyanya.
Hadi kufikia karne ya 20, nyanya zilitumika kutengeneza piza, maji ya
tunda hilo yanatumika kwa mchuzi na hadi sasa zinapendwa ulimwenguni
kote. Mbegu zake zinaweza kustawi bila udongo wenye rutuba hata ukiwa
katika mfuko wa plastiki. Bustani za nyanya zinazotunzwa vizuri
zimestawi tangu enzi za kale kabla ya kuzaliwa Kristo. Jamii ya wafugaji
wanaoishi katika jangwa la Jabaliyyah, wanaotawanyika kwenye milima ya
Sinai wamelima bustani za nyanya zinazomwagiliwa maji kutoka kwenye
vijito na visima vya kuhifadhia maji.
Bustani hizo za wafugaji huzaa nyanya kubwa zinazosafishwa vizuri na
kukaushwa juani kwa ajili ya matumizi wakati wa majira ya baridi kali.
Mimea ya nyanya hujichavisha yenyewe, hivyo aina mbali mbali za nyanya
zinaweza kuzalishwa kutokana na uamuzi wa mkulima kwamba ni aina gani
anapanda kufuatana na matakwa ya wanunuzi na walaji. Hadi sasa kuna aina
4,000 za nyanya hivyo wakulima wanaweza kuchagua ni aina gani
wastawishe.
Aina ya nyanya ndogo nyekundu zilizo na maji mengi huongeza rangi na
ladha kwenye Saladi au Kachumbari, na zile nyanya tamu zenye umbo la yai
mara nyingi hupendelewa zaidi kuhifadhiwa kwenye kopo kwa ajili ya
kusafirishwa kibiashara. Nyanya kubwa zinatumika katika mapishi ya
Kihispania na pia katika upikaji mwingine wa vyakula. Nyanya zinalimwa
ulimwenguni kote, na kila mwaka takribani tani milioni 100 za zao hilo
zinavunwa.
Ingawa nyanya zinajumuishwa katika chakula kiitwacho mboga, kwa
mujibu wa elimu ya mimea, nyanya ni tunda kwa sababu sehemu yenye mbegu
ndiyo inayoliwa na kwa kawaida, sehemu za mboga inayoliwa ni shina ,
majani, na mizizi. Tunda la nyanya lina rangi ya asili iitwayo
“lycopene” inayozuia kuharibiwa kwa chembe kwa sababu ya kuongeza hewa
ya Oksijeni .
Kwa mujibu wa Kitabu cha Kumbukumbu za Dunia “The Guinness Book of
The Records”, tunda kubwa zaidi la nyanya kuwahi kurekodiwa lilipandwa
na lilipovunwa huko Oklahama , Marekani lilikuwa na uzito wa kilogramu
3.5 . Jambo la kuzingatiwa katika kilimo cha nyanya ni kuwa kuvuta
sigara karibu na mimea ya nyanya au kuishika baada ya kuvuta sigara,
kunaweza kuidhuru. Sigara ina virusi vinavyoathiri mmea wa nyanya na
hata mimea mingine.
Tunda la nyanya lina manufaa mengi kwa mwanadamu ikiwemo vitamini A
na C. Uchunguzi uliofanywa unaonesha kwamba chakula kilichopikwa kwa
kutumia rojo na mchuzi wa nyanya nyingi kinaweza kupunguza hatari ya
kupata saratani. Tunda la nyanya linapendwa kwa sababu nyingi ikiwemo
ladha yake inayoweza kuongeza utamu katika chakula , kufanya kachumbari
ivutie , na kuongeza utamu kwenye mchuzi.
Sign up here with your email