Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe amefariki dunia baada ya helikopta aliyokuwa akiitumia kwaajili ya kampeni kupata ajali.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Silaa ambaye pia amempoteza baba yake kwenye ajali hiyo.
“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajiali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha,” ameandika Silaa.
“Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa,nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe.Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani. Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi,” ameongeza.
By Jerry Silaa:

Ajali hiyo imetokea jana jioni ambapo Capt.William Silaa akiwa na Mhe. Deo Filikunjombe na abiria wengine walikuwa kwenye helikopta hiyo iliyo anguka kwenye msitu wa Selous yenye namba 5Y-DKK wakitokea Dar kuelekea Ludewa.
“Usiku kucha vyombo vyote vya serikali vimeendelea na jitihada za kufika eneo la tukio na jitihada kubwa zaidi zinaendelea asubuhi hii,” Silaa aliandika kabla ya taarifa ya watu hao kupoteza maisha.
Sign up here with your email