Zimesalia siku takriban 19 kabla ya Watanzania kupiga kura kwenye uchanguzi mkuu utakaofanyika October 25 mwaka huu.
Dokta Ali Mohammed Shein ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Dokta Ali Mohammed Shein ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Rais
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,anatarajia kutetea kiti chake na
kumaliza muhula wa pili wa uongozi wake, kwa mujibu wa sheria.
Dokta Ali Mohamed Shein alizaliwa machi 13, 1948. Amehitimu katika fani ya Biokemia ya Utabibu kutoka Chuo kikuu cha Odessa nchini Urusi na pia kupata elimu zaidi Uingereza.
Waswahili
wanasema nyota njema honekana asubuhi, kwa dokta Shein umahiri wake
katika uongozi ulianza kuonekana bado akiwa kijana mdogo, kwani mbali na
mbio zake kisiasa kuanza pale alipojiunga na Umoja wa Vijana wa chama
cha Afro-Shirazi wakati akiwa shule, pia alikuwa na kipaji kingine cha
uongozi, katika sekta ya michezo.
Dokta Mohammed Saleh Jidawy ni Katibu mkuu Wizara ya Afya Zanzibar na alisoma na dokta Shein katika shule ya Lumumba, Unguja.
Anasema enzi zake, Dr Shein alikuwa mwanariadhaa hodari mpaka kuwa nahodha katika timu ya shule ya riadha.
Harakati zake kisiasa zinaonekana kuanzia wakati wa
ujana wake,ambapo vijana wengi wa kiafrika walikosa nafasi ya kupata
elimu, na katika misingi hiyo alianza shughuli zake za kijamii, kwa
kushiriki pia kutoa elimu kuwezesha vijana kujielewa, hususan kielimu na
kujiandaa kisiasa kupitia chama chake cha siasa cha Afro Shiraz.
Kutokana na nafasi hiyo aliteuliwa kwenye Kamati Kuu ya CCM 2005.
Alishinda Kiti cha Uwakilishi cha Mkanyageni katika uchaguzi mkuu wa Novemba 6, 2000 na kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora, Novemba 22, 2000.
Nafasi ambayo pengine ilifungua njia zaidi kwa yeye kupanda juu kiuongozi
Kisiasa
zaidi alifahamika Julai 13, mwaka 2001, wakati Dokta Shein alipoteuliwa
kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufanya kazi
pamoja na Rais wa wakati huo Benjamin Mkapa.
Annet Mtawali
Ngahyoma ni mmoja ya waliobahatika kufanya kazi na Dokta Shein mara tu
alipoteuliwa kuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anamuelezea kuwa ni mpole na mwenye kupenda dini.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, Dokta Mohammed Shein
aliteuliwa kuwa mgombea mweza kupitia Chama cha Mapinduzi, Na hatimaye
kuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuapishwa 21
Desemba, 2005, baada ya CCM kuendelea kuongoza nchi.
Kwa mara ya
kwanza aligombea nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Uchaguzi mkuu wa
Oktoba 31 mwaka 2010 na kushinda, hivyo kuapishwa kuwa rais wa Zanzibar
na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Novemba 3 mwaka 2010.
Dokta
Shein ni mtu mwenye msimamo asiyeyumbishwa katika kile anachokiamini, na
hata kuonekana kiongozi imara aliyeweza kuongoza serikali ya Umoja wa
Kitaifa, bila ya kuterereka licha ya shutuma alizotupiwa toka pande
zote.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2015, Dokta ali Mohamed
Shein anawania tena kiti hicho ikiwa ni muhula wa pili na wa mwisho kwa
mujibu wa sheria.
Sign up here with your email